question
stringclasses
5 values
answer
stringclasses
5 values
context
stringclasses
5 values
story_id
stringclasses
5 values
Pengo alimhonga nani
mhuni mmoja
Pengo adaiwa nauli na wanafunzi, inabidi akimbilie msaada wa mkewe Ni muda sasa tangu Sindwele afike Sidindi kumtafuta Pengo. 聭Lazima atakuwa ameshaambiwa kuwa nimekuwa nikimtafuta. Mbona yeye hajajaribu kunitafuta?聮 Sindwele alijiuliza na kushangaa iwapo mwenzake huyo naye alikuwa akiugua yale maradhi ya walimu na wafanya kazi wa shule kubwa kuwapuuza wenzao wa shule ndogo. Huku kimya chake kikistaajabiwa na mwenzake, Pengo alikuwa shuleni Sidindi akihangaikia masuala ya kutamatisha muhula. Ulikuwa wakati wa kufunganya shughuli za muhula. Wapo waliohangaika usahihishaji wa mitihani, wengine walikuwa wanawaandalia wanafunzi mazoezi ya kufanyia nyumbani. Kubwa na zito zaidi kwa Pengo na baadhi ya walimu ni kuwa baadhi ya watoto waliwajia walimu wao wakitaka nauli. Katika mazingira magumu kama haya, hakuna aliyekumbuka kuwa Sindwele nao waliishi katika ulimwengu huu. Alikumbuka vyema alipopewa hela hizi mwanzoni mwa muhula huo. Alizipokea hela kwa ujasiri akitarajia kuwa angewarejeshea hela zao akishalipwa na baraza la mitihani nchini. Hatukutarajia kabisa kuwa ungefika wakati huu kama baraza la mitihani halijalipa. Yaelekea kuwa pesa alizodai baraza zilikuwa zimeingia katika orodha ya vile viendavyo kwa waganga ambavyo havirejei. Mambo kangaja haya. Akalazimika kutafuta mkopo ili awalipe watoto wa wenyewe. Alijaribu kutafuta mikopo kupitia simu lakini hakufanikiwa kwani huko kote alikuwa kakopa. Alikuwa hata kachelewa kulipa baadhi ya madeni na hata akaingizwa kwenye orodha ya wadeni wabaya wasiofaa kukopeshwa chochote. Ilimbidi amhonge mhuni mmoja ili kumwondoa kimagendo kwenye orodha hiyo, sasa angeweza kuomba mkopo tena. Kwa bahati mbaya, alikuwa kakopa katika taasisi zote alizozijua. Alijaribu kuomba mkopo katika shirika la mikopo kwa walimu ila akaambiwa kuwa mshahara wake haungeweza kustahimili mkopo mwingine. Atalazimika kumtafuta mhuni mwingine kwenye tume ya huduma kwa walimu ili amrekebishie stakabadhi zake za mshahara ili aweze kuchukua mkopo mwingine. Punde akagundua kuwa hata huko kurekebishiwa stakabadhi za mshahara hazingemtatulia tatizo lake. Tatizo kubwa hasa lilikuwa kupata wadhamani wa mkopo wake. Kila aliyeulizwa alisema kuwa alikuwa anajiondoa kwenye shirika la mikopo kwa walimu. 聯Wana mafamba sana hao mabwana. Siwezi kuendelea kuyanenepesha matumbo yao na pesa zangu. Watafute wajinga kwingineko.聰 Mwalimu mmoja alilalamika. 聯Shirika la mikopo kwa walimu liko hali mahututi ndugu yangu, linasubiri tu kuzikwa.聰 Mwalimu mwingine alimjuza Pengo. Kimsingi, mwalimu Pengo hakubahatika kumpata mtu au shirika la kumtoa kwenye lindi alimojikuta. Hatimaye, mwalimu wa watu akakumbuka kuwa ng聮ombe akiumia malishoni, hujikokota kurejea nyumbani kwao akasaidiwe, akaamua kumwendea mkewe kwa msaada wa hela.
3862
Majirani walipomwona mtoto, wote walifanya nini
Walirudi nyuma
锘縈toto Punda Siku moja, msichana mdogo aliona umbo la ajabu kwa umbali. Umbo hilo lilipokaribia, aligundua kwamba lilikuwa mwanamke mja mzito. Kwa ushupavu, msichana huyo alimkaribia yule mwanamke mja mzito. Jamaa zake wakasema, "Hatuna budi kumkaribisha akae nasi. Tutamlinda hadi atakapomzaa mtoto wake." Baadaye, mama huyo alikuwa tayari kujifungua. Majirani wakashughulika. "Sukuma! Leta blanketi! Maji! Suukuumaaa!" Mama alijifungua. Majirani walipomwona mtoto, wote walirudi nyuma kwa mshtuko. "Punda!" Wakaanza kugombana. "Tulikubali kuwa tutamlinda huyu mama hadi atakapojifungua, na hivyo ndivyo tutakavyofanya," kiongozi wao alisema. "Hapana! Tukifanya hivyo tutapata bahati mbaya!" alisema jirani mwingine. Mama yule alijikuta peke yake tena. Akajiuliza, "Nitafanyaje na mtoto huyu mwenye kunifedhehesha?" Hatimaye, alikubali kuwa huyo ni mtoto wake na yeye ndiye mamake. Mtoto punda angalibaki alivyozaliwa, mambo yangekuwa tofauti. Lakini, alikua, akakua, hadi mamake akashindwa kumbeba mgongoni. Mamake mara nyingi alichoka na kuvunjika moyo. Mara nyingine mtoto punda alimfanyisha kazi za kinyama. Mtoto punda alikasirika akachanganyikiwa. Hangeweza kufanya lolote kama binadamu. Hakufanana na huyu wala yule. Alizidi kukasirika hadi siku moja akampiga mamake teke akaanguka chini. Mtoto punda aliona aibu. Akakimbilia mbali kadiri alivyoweza. Aliendelea kukimbia hadi usiku alipotambua kuwa amepotea. "Hi ho?" Alinong'ona gizani. "Hi ho?" Mwangwi ukamrudia. Alijikunja mahali akalala usingizi wa mang'amung'amu. Kulipokucha, mtoto punda aliamka na kumkuta mzee wa ajabu akimtazama. Naye pia akamtazama mzee machoni kwa hisia za matumaini. Mzee akasema, "Njoo twende kwangu." Mtoto punda alikubali mwaliko wa mzee huyo. Mzee alimfundisha njia nyingi za maisha. Mtoto punda alijifunza mengi. Asubuhi moja, mzee alimwomba mtoto punda ambebe hadi kilele cha mlima. Walipofika juu mawinguni, walilala. Mtoto punda akaota kuwa mamake alikuwa mgonjwa na alikuwa anamwita. Alipoamka, mawingu yalikuwa yametoweka na mzee rafikiye alikuwa hayupo. Hatimaye, mtoto punda alifahamu atakavyofanya. Mtoto punda alirudi nyumbani akamkuta mamake amenuna. Mama na mtoto wake mpotevu walitazamana kwa muda mrefu. Halafu wakakumbiatiana bila legezo. Mtoto punda na mamake waliishi pamoja kwa ushirikiano. Waliishi kwa furaha pamoja na majirani wao. You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way: Mtoto Punda Author - Lindiwe Matshikiza Translation - Translators without Borders Illustration - Meghan Judge Language - Kiswahili Level - First paragraphs 漏 Text: Lindiwe Matshikiza, Artwork: African Storybook Initiative 2015 Creative Commons: Attribution 4.0 Source www.africanstorybook.org Original source www.donkeychildprojects.org
2328
Ni vipi binti Kidawa alipoteza usichana wake
Kwa kupachikwa mimba
ASIYESIKIA LA MKUU HUVUNJIKA GUU Binti Kidawa alikuwa msichana wa kipekee katika familia ya Bwana na Bibi Hamida. Alikuwa msichana wa mcha mungu sana alimpenda mungu sana kwani alienda kanisani kila siku na maombi yasiyo kwisha. Alikuwa kidato cha nne akisubiria mtihani wake wa kitaifa. Darasani alikuwa namba moja kwani wengi walimsifia sio walimu, wazazi na hata wanafunzi wanzake. Alifanya kazi zote za walimu kwa wakati ufao na alitaka kujua mengi asiyoyafahamu kwajili ya kuhitimu katika kidato cha nne. Binti Kidawa alikuwa msichana mtiifu kwa wazazi na pia walimu kwani alifanya kazi zote alizoagiziwa na mamake wakiwa nyumbani. Alisifiwa na kila mtu apitae kwani watu walimpenda sana Binti Kidawa. Binti Kidawa alipomaliza kidato cha nne huku akisubiria majibu yake ya kidato cha nne, alianza kubadilika ghafla kwani mgema akisifiwa tembo hulitia maji. Kwamba Binti Kidawa alijiona amekua na pembe zimeanza kutokea kwani mama yake alimkanya kwa mienendo na marafiki aliyokua ametangana nao. Lakini wapi, kwani alikuwa kama asiyesikia la mwadhini wala mteka maji msikitini . Hivyo basi Binti Kidawa hakusikia la mama yake na wazazi wake ila aliendelea kufanya alichokuwa akiendelea. Alikanywa wala hakukanyika, aliambiwa wala hakusikia kilicho baki tu wazazi wake walimuacha afunzwe na ulimwengu kwamba sikio halisikii dawa. Mchovya asali huchovya mara nyingi Binti Kidawa aliyekuwa msichana mtiifu kila aina ya sifa alipewa yeye kwamba alikuwa na heshima na kumpenda mungu. Kwani Binti Kidawa alikuwa amekwisha poteza maisha yake. Naam, baada ya mwezi moja, Binti Kidawa alianza kutapika tapika na kutema mate huku alikuwa amekonda kakondeana kama sindano iliyokuwa kitandani tu. Urembo aliyokuwa nayo Binti Kidawa alikuwa hauonekani tena, amebaki kama mifupa tu. Naam, licha kuwa Binti Kidawa alikuwa mwerevu darasani na mwenye mcha mungu na kupenda wazazi wake na walimu amebaki tu akilialia kwa kutosikiza wazazi wake. Kwani hivyo basi alikuwa ameambukizwa ugonjwa wa kutamaucha wa ukimwi na pia alipachikwa mimba. Fahamu hayo Binti Kidawa alipoteza usichana wake na kwa kutojuwa cha kufanya kwani mtoto msikilivu haambiwi di. Binti Kidawa sasa amebaki kulialia tu, hana la kufanya wala lakutenda Ama kweli asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
3191
Hapo awali ni nini kilisababisha ajali
ulevi na mihadarati
MJADALA KUHUSU NAMNA MBALIMBALI ZA KUPUNGUZA AJALI ZA BARABARANI NCHINI KENYA Ajali ni kadhia lenye madhara mengi na hutokea ghafla. Ajali huwa haitokei kisadfa bali hutokea kwa sababu ya binadamu kupuuza mambo fulani. Ajali za barabarani husababishwa na kutofuata alama za barabarani, kutotia sheria za uendeshaji gari barabarani, kupuuza kwa madereva wengine na uendeshaji gari bila ya vyeti wala tajiriba ya uendeshaji gari. Aidha ajali husababishwa na ubovu wa magari na kutowajibika kwa madereva, watembeaji na waendeshaji pikipiki. Kuna aina nyingi za ajali za barabarani. Mathalani ajali za baiskeli, ajali za malori, ajali za bodaboda , ajali za mikokoteni, ajali za matatu, ajali za gari ndogo na ajali za mabasi. Ajali nyingi hutokea nchini Kenya. Unajua kisa na maana? Hata hivyo, penye nia pana njia, ajali za barabarani nchini Kenya zinaweza kupunguzwa kwa kutumia mikakati ifuatayo: Awali kabisa ajali hutokea kwa sababu ya ulevi na matumizi ya mihadarati mengine. Ulevi humfanya binadamu aone vitu mara mbili na kumfanya awe kama amelala yaani mlegevulegevu asiyeweza kutoa uamuzi wa dharura. Mambo haya humfanya dereva asababishe ajali aidha agonge gari au binadamu mwenzake au gari lipinduke. Mlevi anapoendesha gari hujipatia ushupavu na ushujaa nadra. Hayo humfanya dereva awe na mwendo kasi wa ajabu. Mwendokasi ni sababu kuu nchini Kenya ya kutokea kwa ajali. Watu wengi hupenda kusema kuwa wanaharaka na haraka zao huwapeleka jehanamu pasi na kujua kuwa mwendokasi wakati mmoja. Mwendo kasi unaweza kuthibitiwa kwa kueka vituo vya ukaguaji wa ratiba za magari ya abiria. Vilevile kutofuata alama za barabarani ni sababu nyingine inayopandisha idadi ya ajali barabarani. Wizara ya uchukuzi na miundo msingi imeweka mabango barabarani kuonyesha kasi inayofaa au jihadhari na utelezi wa barabara ilhali watu hawafuati haya hupunguza idadi hizi magari yote sharti yatiwe yadhibiti mwendo na wizara ya uchukuzi ihimizwe iwe ikiyakagua kila kuchao. Vyombo vya chakavu kutokana na hali ngumu ya maisha limechangia sehemu kubwa kwa sababu ya ajali nchini. Mtu anaweza kupeleka gari lake gereji na kulipa pesa kidogo na mekanika hao wamwekee vyombo chakavu kwa kuwa amewalipa pesa kidogo. Baada ya ajali watu wengi husema kuwa breki ya gari hilo ilikuwa imekataa kufanya ndiposa ajali ikatokea. Kwa kuepuka hili serikali ipunguze bei ya bidhaa za magari. Katika nchi yetu ya Kenya kila mahali pana barabara mbovu si Machakos, si Kiambu, si Nakuru, si Naivasha wala Mombasa. Barabara huwa na mabonde na huwa zina mashimo na kusababisha ajali. Barabara hizi huwa na kasoro hizi maana hazijakarabitiwa kukaa muda mrefu. Serikali inaweza kupunguza ajali kukikarabati kila mara na kuweka matuta katika kila barabara. Hata pia barabara kuwa finyu husababisha ajali barabarani maana magari huwa mengi na pia kila mmoja huwa na haraka zake. Kila mtu atataka kuwania na kusababisha mgongano wa magari na vifo kutokea. Lazima barabara zipanuliwe kwa sababu za kupunguza msongamano wa magari. Jambo lingine linalosababisha ajali na wasimamia sheria kutotaka ushirikiano. Wasimamia sheria hufika muda na kugoma kufanya kazi mpaka wapewe hongo au bakshishi. Jambo hili linaweza kusababisha upitaji wa vifaa haramu na hata pia madawa ya kulevya. Serikali inaweza kupunguza hili kwa kutuma wachunguzi wa kuwafuatilia wasimamizi wa sheria wanaotaka hongo na kuadhibiwa vikali na hata pia kufutwa kazi. Vilevile udereva bila mafunzo ya taaluma ya kuendesha magari husababisha ajali. Watu wengi huona kuwa wanaweza kuendesha gari bila mafunzo, hujiona kuwa wameshakuwa bingwa ilhali hajui mambo mengi ya barabarani. Nchini Kenya kuna vyuo vikuu vinavyo fundisha taaluma hii kama UNIK, NDOVU, AA, ISTIQAMA na BUDGET mtu kujisajili huona ni upotevu wa muda. Kuepuka ajali madereva wasome taaluma ya uendeshaji wa magari kwa lazima. Hata hivyo pia giza usiku husababisha ajali. Magari huwa na taa za mbele na nyuma lakini huwa hazikidhi haja vizuri. Baada ya saa kumi na mbili jioni hujulikana kuwa duniani huwa mna giza totoro. Basi giza hilo linaweza kusababisha ajali kubwa. Kutotaka kutokea kwa ajali serikali itengeneze mataa makubwa barabarani ili kuepuka vifo vya watu wasio na hatia. Kubeba abiria zaidi ya kiwango cha kawaida pia hueza kusababisha ajali. Hasahasa katika daladala wakati huu wa uviko wa Covid 19, watu au abiria wanafaa wasizidi zaidi ya wanane ilhali daladala kadhaa zinaweza kubeba zaidi ya wanane ili wapate pesa kiurahisi bila ya kujua au kupuuza kuwa wanasambaza uviko huu wa covid-19. Serikali inaweza kupunguza ajali kwa kueka usimamizi wingi na kuwaeka kila kituo ili kuangalia magari yanayokiuka sheria hiyo. Kabla ya kalamu yangu kuisha wino ningependa kuwaambia serikali kuzikarabati barabara kila mara, kuzifanya barabara kuwa kubwa, kuzifanya alama za barabarani kuonekana, kujenga matuta barabarani na kuwalipa wasimamia sheria wakati mwafaka. Vile vile madereva wapewe sheria zinazokataza ulevi, kutoendesha kwa mwendo wa kasi, wafuate alama za barabarani , madereva wa pikipiki na abiria wake wote wavae helmeti na kutoendesha magari usiku路 Abiria pia wasikimbilie magari, wafunge mishipi wakiwa safarini na wanaotembea kwa miguu wajengewe vipitio vya juu.
0171
Matawi ya Mtende yalitumika kufanya nini
Kuezeka paa za vyumba
锘縈hogo na Mtende Hapo zamani, Mhogo na Mtende waliishi kijijini Koowa. Kama marafiki, walitembeleana kila siku. Walikuwa wakulima waliofanya kazi kwa bidii katika mashamba yao. Katika mwaka mmoja, kulikuwa na ukosefu wa mvua. Mimea yote ilikauka. Watu wakakosa chakula. Mhogo na Mtende waliamua kwenda kutafuta kazi katika kijiji tofauti. Wlimkuta mwanamke mmoja wakamsalimu, "Hujambo?" Aliitikia kisha akwauliza, "Mnakwenda wapi?" Mtende alimjibu, "Tunakwenda kutafuta kazi katika kijiji jirani." "Kazi gani mnayofanya?" Mwanamke yule aliuliza. Walijibu, "Tunaweza kuipa chakula familia yako na mifugo wako. Mwanamke alwauliza tena, "Mtahitaji nini kutupatia chakula hicho?" Walimjibu, "Tupe ardhi, maji na huduma nzuri." Mwanamke yule aliwapeleka nyumbani kwake. Alasiri moja, Mtende na Mhogo walibishana vikali. Mhogo alisema kuwa yeye alikuwa muhimu zaidi kuliko Mtende. Mtende naye akasema kuwa yeye alikuwa muhimu kuliko Mhogo. Mwanamke yule aliwasikia kutoka chumbani kwake. Alitoka nje na kwauliza, "Mbona mnabishana?" Mhogo alikuwa wa kwanza kuzungumza. "Mimi ni muhimu zaidi kuliko Mtende. Ninazaa mihogo mnayotumia kutengeneza fufu na unga wa mihogo." "Watu hupanda mashina yangu. Mifugo wenu hula majani na maganda yangu. Je, Mtende hufanya nini?" Mhogo aliuliza. Mtende alicheka, akatikisa kichwa chake kisha akasema, "Mwanamke wee, unaikumbuka supu ya tende unayofurahia sana? Hutoka kwa nani?" 10 "Mimi hutoa mafuta yanayotumiwa kukaanga samaki na nyama. Je, utawezaje kutayarisha kitoweo na mchuzi bila mafuta?" "Zaidi ya hayo, matawi yangu huezeka paa za vyumba vyenu na vibanda vya kupumzikia. Mnaburudika baada ya kazi kwa kuinywa kosha ninayotoa." "Isitoshe, fagio zinazotumiwa kufagia vyumba na uwanja wa nyumba zenu zinatoka kwangu," Mtende alimaliza kusema. "Hmmm!" Mwanamke alizusha pumzi. "Ni sawa marafiki, nimewasikia. Nitaitatua shida hii." "Ninyi nyote ni viumbe muhimu sana kwangu. Pamoja, mnatengeneza mlo mtamu wa fufu na supu ya tende!" mwanamke akasema. Mwanamke yule alitayarisha supu ya tende pamoja na fufu kutoka kwenye mihogo. Aliwaalika marafiki zake kula naye. Walifurahia chakula hicho sana. Tangu wakati huo, Mhogo na Mtende wamekuwa marafiki wakubwa. You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way: Mhogo na Mtende Author - Divine Apedo, Elizabeth Nkrumah and Georgina Abbey Translation - Ursula Nafula Illustration - Brian Wambi Language - Kiswahili Level - First paragraphs 漏 African Storybook Initiative 2017 Creative Commons: Attribution 4.0 Source www.africanstorybook.org
2308
README.md exists but content is empty.
Downloads last month
38